PSG na Madrid uso kwa uso

0
152

Droo ya ratiba ya michezo ya hatua ya 16 bora ya Ligi ya Mabingwa barani Ulaya imefanyika hii leo ambapo mchezo unaosubiriwa kwa hamu ni ule wa miamba ya Ufaransa PSG dhidi ya mabingwa wa kihistoria wa michuano hiyo Real Madrid.

Mchezo mwingine utawakutanisha miamba kutoka Hispania Atletico Madrid dhidi ya Mashetani wekundu Manchester United, Chelsea watakutana na Lille kutoka Ufaransa huku Inter Milan wakivaana na Liverpool.

Michezo raundi ya kwanza itachezwa tarehe 15-23 Februari 2022, na mzunguko wa pili utachezwa Machi 8-16 2022.