Wajela jela kutoka Jijini Mbeya Tanzania Prisons wataikaribisha Yanga SC ya Dar es Salaam katika mchezo wa Ligi Kuu Vodacom Tanzania Bara kwenye uwanja wa Samora Mjini Iringa
Hapo awali mchezo huo ulipangwa ufanyike Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya lakini baada ya taarifa ya TFF sasa mchezo huo utafanyika kesho Uwanja wa Samora mjini Iringa.
Yanga SC ipo mjini Mbeya tangu Jumapili na Jumanne ikicheza mechi yake ya kwanza ya Ligi Kuu dhidi ya wenyeji Mbeya City na kutoa sare ya bila kufungana.