Polisi Tanzania yazidi kujichimbia shimo

0
246

Hali ya Polisi Tanzania inazidi kuwa mbaya wakiwa mkiani mwa Ligi Kuu ya NBC baada ya leo kushindwa kutumia vizuri uwanja wa nyumbani kwa kulazimishwa suluhu na Wana Nkurukumbi, Kagera Sugar.

Maafande hao wa Polisi wapo katika nafasi ya 16 wakiwa na alama 16 baada ya kushuka dimbani mara 22, huku mkakati wao wa kujinasua kutoka kwenye madhila ya kushuka daraja ukionekana kutoleta matunda tarajiwa.

Suluhu ya leo imeipandisha Kagera Sugar hadi nafasi ya nane ikifikisha alama 26 baada ya kushuka dimbani mara 22.

Katika michezo 10 ya ligi, Polisi Tanzania wamepata ushindi kwenye mchezo mmoja tu huku Kagera Sugar ikishinda michezo mitatu.