Klabu ya Soka ya Tottenham Hotspur imemfuta kazi kocha wake Mkuu Mauricio Pochettino huku taarifa kutoka klabuni hapo zikisema wanafikiria nani atachukua mikoba ya Pochettino

Licha ya kufika fainali ya Ligi ya Mabingwa msimu uliopita Tottenham imeanza vibaya katika Michuano ya Ligi kuu England msimu huu ikiwa nafasi ya 14 alama 14 huku ikiwa imeshacheza michezo 12.
