Pochettino aelezea mchezo wa Tottenham na Bayern Munich

0
1093

Kocha wa timu ya Tottenham Hotspur, – Mauricio Pochettino amesema kuwa, timu yake ilipoteza ari na kukata tamaa ya mchezo baada ya kuruhusu bao la Nne kwenye kipigo cha mabao Saba kwa mawili ilichopata mbele ya Bayern Munich.

Pochettino anaamini baada ya timu yake kupata bao la Pili na kufanya ubaousomeke mabao Manne kwa Mawili, mambo yalibadilika na timu yake ingeweza kupata walau sare, lakini walipoongezwa bao la Tano timu yake ikanyong’onyea zaidi na kutoka mchezoni.

LONDON, ENGLAND – NOVEMBER 02: Mauricio Pochettino manager of Tottenham Hotspur gives instructions during the Barclays Premier League match between Tottenham Hotspur and Aston Villa at White Hart Lane on November 2, 2015 in London, England. (Photo by Mike Hewitt/Getty Images)

Wakiwa kwenye uwanja wao wa nyumbani wa Tottenham Hotspur jijini London nchini Uingereza,- Tottenham ndiyo walikuwa wa kwanza kupata bao mapema kwenye kipindi cha kwanza kupitia kwa Heung-Min Son katika dakika ya 12 kabla ya Bayern Munich hawajasawazisha dakika tatu baadaye kupitia kwa Joshua Kimmich aliyefunga kwenye dakika ya 15, kisha Robert Lewandowski akaifungia Bayern bao la Pili kwenye dakika ya 45 na mchezo kwenda mapumziko Bayern wakiwa mbele kwa mabao mawili kwa moja.

Bayern wakakianza kwa kasi kipindi cha pili ambapo Serge Gnabry akaifungia timu yake mabao mawili ya haraka kwenye dakika ya 53 na 55 kabla Harry Kane hajafunga bao la Pili kwa upande wa Tottenham Hotspur katika dakika ya 61.

Bayern wakaongeza mabao mengine Matatu ya haraka katika dakika ya 83, 87 na 88 yakitiwa kimiani na Serge Gnabry aliyefunga mawili na kufikisha mabao manne kwenye mchezo huo huku bao lingine kwenye dakika hizo za mwisho likifungwa na Robert Lewandowski aliyefunga mabao mawili hapo jana.

Kichapo hicho cha mabao Saba kwa Mawili kwenye mchezo wa kundi Be, kinakuwa kichapo kikubwa zaidi ilichowahi kukumbana nacho Tottenham Hotspur ikiwa kwenye uwanja wake wa nyumbani katika mashindano ya Kimataifa.

Mchezo mwingine wa kundi Be umeshuhudia Red Star Belgrade ya Serbia ikiinyuka mabao Matatu kwa Moja timu ya Olympiacos ya Ugiriki.