Nguli wa Soka wa Brazil, Edson Arantes do Nascimento, maarufu Pele (82) amefariki dunia.
Amefariki wakati akipatiwa matibabu ya saratani katika moja ya hospitali nchini Brazil tangu Novemba mwaka huu.
Pele anayetambulika kama mchezaji bora kuwahi kuwepo, alifunga magoli 1,281 kwenye michezo 1,363 katika miaka 21 ya uchezaji soka.
Aidha, ndiye mchezaji pekee ambaye ameshinda Kombe la Dunia mara tatu, mwaka 1958, 1962 na 1970, ambapo mwaka 2000 alitawazwa kuwa mchezaji bora wa karne.