Pele aagwa, kuzikwa leo

0
137

Mwili wa gwiji wa soka wa Brazil na mchezaji bora wa wakati wote ulimwenguni, Edson Arantes do Nascimento almaarufu Pele umeagwa siku ya jana na leo ndio maziko rasmi yanafanyika huko katika mji wa Santos nchini Brazil.

Rais wa Brazil alitangaza siku tatu za maombolezo ya kitaifa ili kutoa heshima kwa gwiji huyo wa soka na leo mwili wake utapumzishwa pembezoni mwa uwanja wa Santos ambapo Pele amechezea klabu hiyo kwa zaidi ya miaka 20.

Wakati wa shughuli ya kuaga mwili wa pele, wachezaji na viongozi wa Santos ndio waliohusika na ubebaji wa jeneza lililohifadhi mwili wa Pele kabla ya mamia ya waombolezaji kutoa heshima zao za mwisho kwa saa 24.

Kabla ya maziko yake hii leo jeneza litatembezwa katika mitaa ya Santos na kupita mbele ya nyumba ya mama yake mzazi, Celeste, ambaye ana umri wa miaka 100.