NUSU FAINALI UEFA NI VITA YA ENGLAND NA HISPANIA

0
823

Timu mbili za ligi kuu England zimepenya hatua ya nusu fainali ligi ya mabingwa barani ulaya licha ya kutoa sare katika michezo yao ya mwisho kwenye hatua ya robo fainali, huku timu mbili kutoka La Liga zikiwasubiri vinara hao wanaochuana vikali katika ligi yao.

Majogoo ya Jiji, Liverpool wamesonga mbele kwa ushindi wa jumla ya mabao 6 kwa 4 dhidi ya Benfica huku Manchester City ikitoka suluhu na Atletico Madrid lakini wakifanikiwa kufuzu hatua ya nusu fainali baada ya kupata ushindi wa bao moja kwa bila katika mchezo wa kwanza uliopigwa katika dimba la Etihad.

Liverpool watakutana na Villareal ya Hispania iliyowatoa Bayern Munich ya Ujerumani kwa mabao 2 kwa 1, huku vinara wa England Manchester City wakikutana na Real Madrid waliokuwa na kibarua kigumu cha kuing’oa Chelsea, ambaye ni bingwa mtetezi wa michuano hiyo, kwa mabao 5 kwa 4 katika mchezo uliofika hadi dakika 120.