Klabu ya Simba, leo itakua nyumbani kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam kucheza na timu ya UD do Songo ya Msumbiji katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Barani Afrika.
Katika mchezo wa kwanza timu hizo zilitoka suluhu ya bila kufungana, Simba ikiwa ugenini.
Kocha wa Simba, -Patrick Aussems amesema kuwa wanajiamini kuwa wataibuka na ushindi kwenye mchezo huo licha ya kukabiliana na timu ngumu.
Amesema timu yake ipo tayari na inajua inataka kushinda na watafanya kila linalowezekana ili kufanikisha hilo.