Ni Jumanne nyingine ya kisasi

0
771

Mwaka 2018 Argentina ilidhalilika dhidi ya Croatia kwa kuruhusu mabao 3-0 kwenye hatua ya makundi ya michuano ya Kombe la Dunia, msimu huu wanakutana katika nusu fainali.

Croatia walioitoa Brazil kwa mikwaju ya penati wapo kwenye kiwango bora sana kimbinu dhidi ya Argentina waliowatoa Uholanzi kwa mikwaju ya penati wakiwa kwenye kiwango cha kupwa na kujaa mchezoni.

Ni Jumanne nyingine ya kisasi

Mabingwa watetezi, Ufaransa wapo kwenye kiwango kizuri, wanakutana na ‘surprise package’ ya michuano hii timu ya Taifa ya Morocco ambayo imekuwa timu ya kwanza kutoka Afrika kufuzu hatua ya nusu fainali.

Wakati Ufaransa ikisifika kwa safu bora ya ushambuliaji hali ni tofauti kwa Morocco wanaosifika kwa safu nzuri ya ulinzi na nidhamu kubwa kiwanjani.

Wametoka sare na Croatia, wamewafunga Ubelgiji, Ureno na kuwatoa vigogo wengine Uhispania. Wapo kwenye kilele cha mafanikio dhidi ya mabingwa watetezi ambao nao wapo kwenye ‘mood’ ya hatari.

Msisimko huu wa nusu fainali zote utaushuhudia mbashara kupitia TBC 1, TBC Taifa na TBCOnline siku za Jumanne na Jumatano kuanzia saa 4 usiku kwa matangazo bora yenye mwonekano ang’avu na watangazaji mahiri kabisa.