Ni JKT Queens au Simba Queens leo

0
588

Pazia la Ligi Kuu ya Wanawake Bara (SWPL) linafungwa leo, huku mvuto ukiwa mkubwa zaidi katika siku ya mwisho kwani michezo itakayopigwa leo ndio itakayoamua nani anakuwa bingwa.

Dakika 90 zitaamua kama JKT Queens wenye alama 43 ndio wanakuwa mabingwa au kombe linakwenda Msimbazi kwa Simba Queens wenye alama 42.

Timu hizo mbili zitashuka dimbani katika viwanja viwili tofauti mkoani Iringa ambapo JKT Queens itacheza dhidi ya Mkwawa Queens huku Simba Queens ikicheza dhidi ya Ceasiaa Queens.

Hata hivyo. JKT Queens inapewa nafasi kubwa zaidi kutwaa ubingwa huo kutokana na kutopoteza mchezo wowote msimu huu, ikiwa imekwenda sare michezo minne, hivyo ushindi wa leo ndio kitu pekee wanachohitaji, huku Simba Queens ikiwa imepoteza mchezo mmoja na kutoka sare mitatu.

Pia JKT Queens wanacheza na Mkwawa Queens ambao tayari wameshuka daraja wakiwa mkiani, huku Ceasiaa Queens inayocheza na Simba Queens ikiwa nafasi sita.