Naomi Osaka apata mtoto

0
199

Bingwa mara nne wa Grand Slam, Naomi Osaka amejifungua mtoto wa kwanza mjini Los Angeles, chama cha tenesi cha wanawake kimetangaza.

Mjapan huyo mwenye umri wa miaka 25 alifichua ujauzito wake mwezi Januari na kusema mwezi uliopita alikuwa anatarajia mtoto wa kike na mpenzi wake ambaye ni rapa, Cordae.

Osaka alicheza kwa mara ya mwisho kwenye Pan Pacific Open huko Tokyo mnamo Septemba 2022.

Mwaka 2021 alishinda tuzo kuu nne kwenye Australian Open mwaka 2021.

Aidha, akizungumza Aprili mwaka huu aliweka wazi kuwa anataka kushinda medali ya dhahabu katika michezo ya Olimpiki ya Paris mwaka ujao.