Mzee Akilimali Afariki Dunia

0
523

Aliyekuwa Mwenyekiti wa Baraza la Wazee wa Klabu ya Yanga Sc Mzee Ibrahim Akilimali amefariki dunia leo alfajiri wilayani Bagamoyo mkoani Pwani.

Ibrahim Akilimali amefariki akiwa anapatiwa matibabu Hospitali ya Bagamoyo, mkoani Pwani ; Ofisa habari wa Yanga, Hassan Bumbuli amethibitisha kupokea taarifa hizo huku klabu ikisubiri taratibu za familia kuhusu taratibu za msiba huo.