Mwili wa Pele kuagwa leo

0
119

Mwili wa gwiji wa soka wa Brazil, Edson Arantes do Nascimento almaarufu Pele utaagwa leo ukiwa katikati ya uwanja wa klabu ya Santos wa Vila Belmiro kwa saa 24.

Mazishi ya gwiji huyo yanatarajiwa kufanyika siku ya Jumanne katika uwanja huo unaotumiwa klabu hiyo ambayo Pele aliitumikia kwa sehemu kubwa ya maisha ya kandanda.

Jeneza lake litatembezwa katika mitaa ya Santos na kupita mbele ya nyumba ya mama yake mzazi Celeste ambaye ana umri wa miaka 100.