Mwenyekiti wa Klabu wa Simba ya jijini Dar es salaam, -Swedi Nkwabi, amejiuzulu nafasi hiyo kwa kile alichokieleza kuwa ni kuhitaji muda zaidi wa kusimamia shughuli zake binafsi.
Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari na uongozi wa klabu hiyo ya Simba imeeleza kuwa, Swedi amefikia uamuzi huo kwa hiari yake na tayari ameiandikia barua Bodi ya Wakurugenzi kuitaarifu juu ya uamuzi wake.
Nao uongozi wa Simba umebariki uamuzi huo na kumuomba aendelee kushiriki katika shughuli mbalimbali za klabu hiyo.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo ya Simba, utaratibu wa kumpata Mwenyekiti mpya atakayejaza nafasi hiyo utatangazwa baadaye.