Bingwa mara tatu wa zamani wa mashindano makubwa ya Tenisi (Glad Slam) – Andy Murry wa Uingereza, amefanyiwa upasuaji wa nyonga jijini London nchini Uingereza.
Murry amekuwa akisumbuliwa na tatizo la nyonga kwa muda mrefu na mapema mwezi huu kabla ya kuanza kwa mashindano ya Wazi ya Tenis ya Australia na alisema kuwa anaweza kustafu kucheza Tenisi katikati ya mwaka huu.
Kupitia ukurasa wake wa mtandano wa kijamii wa Istagram,- Andy Murray ameweka picha akiwa amelazwa hospitalini huku picha nyingine ikionyesha picha ya X-Ray na mwenyewe amesema kuwa ana hakika sasa atakuwa amemaliza tatizo hilo la nyonga lililomsumbua kwa muda mrefu.
Hii ni mara ya pili kwa nguli huyo kufanyiwa upasuaji wa tatizo la nyonga, ambapo mwaka 2018 alifanyika upasuaji na kufanikiwa kucheza michezo 15 baada ya kurejea uwanjani.
Tayari Murry ameshajitoa kushiriki mashindano ya Marseille Open yatakayofanyika mwezi Februari mwaka huu nchini Ufaransa na kwenye mashindano ya Australia Open ya mwaka huu alitolewa kwenye mzunguko wa kwanza na Roberto Bautista Agut wa Hispania.