Meneja wa mchezaji wa kimataifa wa Tanzania na klabu ya Difaa El-Jadidi ya Morocco, Saimon Msuva Jonas Tibhoroha amethibitisha kuwa mchezaji huyo amejiunga na Klabu ya Benfica inayoshiriki ligi kuu nchini Ureno kwa mkataba wa miaka mitatu.
Klabu hiyo itamtoa Msuva kwa mkopo wa miezi sita kwenda klabu ya Panathiakos ya Ugiriki.