Mpira rasmi wa Kombe la Dunia kwa Wanawake 2023

0
168

OCEAUNZ umetambulishwa kuwa mpira rasmi utakaotumika katika mshindano ya Kombe la Dunia kwa Wanawake mwaka 2023.

Mpira huo ambao umetengenezwa na kampuni ya Adidas una teknolojia ya kisasa ambazo zitasaidia katika maamuzi wakati wa mchezo na kukusanya taarifa/takwimu za mchezo husika ambazo makamisaa wa mchezo wataweza kuziona wakati mchezo unaendelea.

Miongoni mwa teknolojia zitakazotumika wakati wa mchezo kwenye mpira huo ni pamoja na kumsaidia mwamuzi kujua endapo mchezaji ameotea (offside).

Muundo wa mpira huo umetokana na mandhari ya mataifa wenyeji wa mashindano hayo ambayo ni Australia na New Zealand, mandhari ambayo yamependezeshwa na milima na bahari.

Mashindano hayo yanatarajiwa kutimua vumbi Julai 20 na kufikia tamati Agosti 20 mwaka huu.