Morrison arejeshwa kikosini

0
2267

Klabu ya soka ya Simba imemrejesha kikosini Mchezaji wake Bernard Morrison ambaye ni Raia wa Ghana baada ya Mchezaji huyo kuomba radhi.

Taarifa iliyotolewa na Simba imeeleza kuwa Mchezaji huyo ameomba radhi kwa CEO wa Simba Barbara Gonzalez, kocha Pablo Franco na benchi la ufundi kwa ujumla.

Simba ilimsimamisha Morrison na kumpa siku 7 za kuandika barua na kueleza kwanini asichukuliwe hatua zaidi za kinidhamu kwa tuhuma zinazomkabili za utovu wa nidhamu.

Siku kadhaa zilizopita mchezaji huyo alionyesha kujutia kitendo cha kinidhamu alichokitenda akiwa kambini baada ya kutuma ujumbe mfupi wa kuomba msamaha kwa wachezaji wenzake na uongozi klabu hiyo kupitia mitandao ya kijamii.