Mkoa wa Mjini Magharibi umeibuka bingwa wa jumla wa mashindano ya kombe la Taifa (Taifa Cup 2021) yaliyomakizika kwenye uwanja wa Mkapa mkoani Dar es Salaam.
Mkoa wa Arusha umekuwa wa mshindi pili wa jumla ukifuatiwa na Dar es Salaam ambayo imeshika nafasi ya tatu.
Mashindano hayo yalishirikisha mchezo wa soka kwa Wanawake na Wanaume, netiboli, riadha, maonesho ya sanaa za muziki wa kizazi kipya pamoja na singeli.
Kwa upande wa soka la Wanaume, mkoa wa Mjini Magharibi ndiyo bingwa ukifuatiwa na Mara na nafasi ya tatu imeshikwa na mkoa wa Ruvuma, huku kwa soka la Wanawake mkoa wa Arusha umeongoza ukifuatiwa na Dar es Salaam na mshindi wa tatu ni Mara.
Mchezo wa netiboli mkoa wa Mjini Magharibi umeshika nafasi ya kwanza ukifuatiwa na Dar es Salaam nafasi ya pili na nafasi ya tatu imechukuliwa na Dodoma, wakati kwenye mchezo wa riadha Kusini Unguja ndiyo bingwa ukifuatiwa na Arusha na Kilimanjaro iliyoshika nafasi ya tatu.
Kwenye maonesho ya sanaa za muziki wa kizazi kipya, Pwani imeongoza ikifuatiwa na Mbeya na Dar es Salaam ni mshindi wa tatu, na kwenye muziki wa Singeli mabingwa ni Morogoro, unaofuata ni mkoa wa Dar es Salaam ambao ni mshindi wa pili na Mjini Magharibi imeshika nafasi ya tatu.