Miss Tanzania ashangazwa na uchimbaji wa Madini

0
2730

Mlimbwende wa Tanzania mwaka 2021 Rose Manfere ameelezwa
kushangazwa na namna shughuli za uchimbaji wa madini zinazofanywa huku
akisifu shirika la Madini la Taifa (STAMICO) kwa namna linavyosimamia
rasilimali hizo.

Mrembo huyo ambaye ametembelea Banda la wizara ya Nishati na Madini na
kujionea shughuli mbalimbali zinazooneshwa na taasisi zilizochini ya wizara
hiyo, amesema, hapo awali hakufahamu namna shughuli za madini
zinavyofanyika.

Kupitia ziara yake hiyo Miss Rose amesema, Shirika la Madini la Taifa
(STAMICO) imeweza kusimamia rasilimal hizo na kuzifanya kuwa na manufaa
kwa taifa.

Mrembo huyo amewata watanzania kujifunza shughuli za uchimbaji wa madini
ili kuzifahamu rasilimali zao na manufaa yake kwa nchi .