Michuano ya vijana yatimua vumbi Poland

0
261

Michuano ya dunia ya vijana wenye umri chini ya miaka 20,  inaendelea kutimua vumbi nchini Poland huku wenyeji wa michuano hiyo ikianza vyema kwa kuitandika timu ya visiwa vya Tahiti mabao matano kwa bila.

Katika michezo mingine, Argentina imeichapa Ureno mabao mawili kwa bila, Korea ya Kusini ikaitandika Afrika Kusini bao moja kwa bila, Mali ikaichabanga Saudi Arabia mabao manne kwa matatu na Ufaransa imeichapa Panama mabao mawili kwa bila.

Michuano hiyo itaendelea siku ya Jumatano kwa kuzikutanisha Ecuador na Mexico, Italia na Japan, Senegal dhidi ya Poland na Colombia itavaana na Tahiti.

Siku ya Alhamisi New Zeland itamenyana na Uruguay, Norway na Hondurus, Nigeria na Ukrine na Marekani dhidi ya Qatar.