Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limesogeza mbele mchezo wa hatua ya nusu fainali ya Kombe la Shirikisho (ASFC) kati ya Singida BS na Yanga SC uliopangwa kuchezwa Mei 7 mwaka huu katika Uwanja wa Liti, Singida hadi hapo utakapopangiwa tarehe nyingine.
Mabadiliko hayo yametokana na maombi ya Yanga SC kuomba kupata muda wa maandalizi ya mchezo wa Nusu Fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika utakaochezwa Mei 10, 2023 mkoani Dar es Salaam.
TFF imesema kuwa mabadiliko hayo yamefanyika kwa maslahi mapana ya nchi.
Aidha, TFF imeusogeza mbele mchezo wa nusu fainali ya ASFC kati ya Azam FC na Simba SC uliokuwa uchezwe Mei 6, 2023 katika Uwanja wa Nangwanda Sijaona, Mtwara, na sasa utachezwa Mei 7, 2023.