Mfahamu Pierluigi Collina

0
119

Pierluigi Collina alizaliwa Februari 13, 1960 huko mjini Bologna nchini Italia.

Collina ni moja ya marefa bora kuwahi kutokea ulimwenguni enzi akichezesha kabumbu alikubalika mno kutokana na uwezo wake wakuzimudu sheria 17 za soka.

Mwamuzi huyu raia wa Italia amechaguliwa na FIFA kuwa refa bora wa mwaka kwa takribani mara sita mfululizo kuanzia mwaka 1998 hadi mwaka 2003 na anatajwa kuwa refa bora wa muda wote Ulimwenguni.

Alitambuliwa rasmi na FIFA mwaka 1995 na alichezesha fainali ya kombe la dunia mwaka 2002 kati ya Brazil na Ujerumani ambapo Brazil ilitwaa ubingwa.

Collin amechezesha michezo mitano ya Kombe la dunia alitangaza kustaafu kazi hiyo mwaka 2005.

Bado siku 12, kaa tayari kutazama na kusikiliza Fainali za Kombe la Dunia kupitia TBC buuree kuanzia Novemba 20 – Disemba 18.