Mchezo wa Yanga na KMC, TPLB yatoa ufafanuzi

0
823

Bodi ya Ligi (TPLB) imesema kuwa hakuna mabadiliko ya uwanja utakaotumika kwenye mchezo kati ya Yanga dhidi ya KMC zote za jijini Dar es salaam, mchezo utakaochezwa Jumapili Machi 10 mwaka huu.

Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi Boniface Wambura amesema kuwa  mchezo huo utachezwa kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam  kama ulivyopangwa na baada ya hapo ndipo kutatangazwa mabadiliko mengine.

Mapema wiki hii kulienea taarifa kuwa mchezo huo ungechezwa nje ya jiji la Dar es salaam kutokana na uwanja wa Taifa kuhitajika katika maandalizi ya michuano ya vijana wenye umri wa chini ya miaka 17.