Mchezaji mwingine wa Tembo Warriors atimkia Uturuki

0
1608

Timu ya Taifa ya wenye Ulemavu, Tembo Warriors inayojiandaa kwenda Kombe la Dunia imeendelea kuvuna matunda kwa wachezaji wake kuchaguliwa kucheza soka la kulipwa kwenye vilabu vinavyo shiriki ligi ya uturuki.

Leo alfajiri wachezaji wa Tembo Warriors wametoa heshima ya kumuaga mchezaji mwenzao Shedrack Hebron aliyechaguliwa kujiunga na club ya Yeditepe mjini Istanbul.

Shedrack anakuwa mchezaji wa pili wa timu ya Taifa kwenda Uturuki baada ya mchezaji wa kwanza Frank Nagilo kupata usajili katika club ya Izmir.

“Tunaendelea kuipongeza Serikali kupitia Wizara ya Michezo pamoja na Baraza la Michezo Tanzania, pia tunawashukuru wadau mbalimbali waliosaidia mchakato wa gharama wakiwemo wabunge wa kamati ya Bajeti,” amesema Peter Sarungi Rais wa TAFF.

Kwa sasa timu ya Taifa Tembo Warriors ipo kambini ikiendelea na maandalizi ya Kombe la Dunia.