Tanzania kuwekeza kwenye michezo

0
201

Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mohamed Mchengerwa amesema Tanzania imefanya mapinduzi makubwa kwenye Michezo katika kipindi kifupi chini ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan.

Mchengerwa ameyasema hayo kwenye mahojiano maalum na kituo kimoja cha Redio nchini Uingereza.

Mchengerwa amesema katika kipindi kifupi Tanzania imefanikiwa kuingiza timu nne kwenye mashindano ya dunia.

Aidha, amesema Tanzania inafanya uwekezaji mkubwa kwenye miundombinu ambapo inatarajia kuandaa mashindano makubwa ya michezo.

Kuhusu mkakati wa kuibua vipaji Mchengerwa amesema tayari imeandaa program ya mtaa kwa mtaa.

Mchengerwa amesema Serikali imefufua mashindano ya michezo kwa shule za msingi(UMITASHUMTA) na Sekondari (UMISETA) ili kuibua vipaji.