Mbeya City yaifunga Simba SC

0
1082

Maafisa wa Jiji la Mbeya, Mbeya City wameondoka na alama tatu katika Uwanja wa Sokoine mkoani humo baada ya kuifunga Simba SC goli 1-0 katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Goli pekee la ushindi kwenye mchezo huo limefungwa na Paul Nonga dakika ya 19 na kufanikiwa kuipandisha Mbeya City hadi nafasi ya tatu ya msimamo ikiwa na alama 19.

Katika mchezo huo Mbeya City wamelazimika kucheza wakiwa pungufu baada ya beki wao Mpoki Mwakinyuke kutolewa kwa kadi nyekundu ikiwa ni njano ya pili.

Kufuatia kipigo hicho, Simba imebaki nafasi ya pili ikiwa na nafasi 24 baada ya kushuka dimbani mara 11. Kipigo hicho pia kimeongeza utofauti wa alama kati ya Simba na Yanga kufikia alama nane, ambapo Yanga inaongoza ikiwa na alama 32.

Timu hizo zitakutana tena Juni 9 mwaka huu ambapo Simba itakuwa na nafasi ya kujiuliza ama Mbeya City kuendeleza ubabe.