Ligi kuu Tanzania bara imeendelea leo katika viwanja mbalimbali nchini, Wekundu wa msimbazi Simba imeshinda bao moja kwa bila dhidi ya Wanapaluhengo Lipuli fc bao pekee la Simba likifungwa na John Boko
Wagosi wa kaya Coastal union imeitandika Azam fc mabao 2 kwa 1 na kujizolea alama 3 muhimu katika uwanja wa uhuru jijini Dar es salaam
KMC imekubali kichapo cha mabao 3 kwa 2 dhidi ya Polisi Tanzania, Mwadui wakitoka sare ya bao 1 kwa 1 dhidi ya Namungo fc
Mtibwa Sugar wamechezeshwa kwata na JKT Tanzania na kutandikwa bao moja kwa nunge, huku Biashara United ikishinda bao moja bila dhidi ya vijana wa Alliance fc
Singida united imechezea kichapo cha bao moja kwa bila dhidi ya Ndanda fc, Ruvu shooting wakitumia vyema uwanja wa nyumbani kwa kuitandika Mbeya City bao moja bila
Kagera sugar imeibamiza Mbao fc mabao 2 kwa bila huku mechi ya mwisho ikimalizika kwa sare tasa baada ya Tanzania Prisons kulazimisha sare hiyo ya bila kufungana dhidi ya Yanga mchezo ukipigwa katika uwanja wa Taifa Dar es salaam