Manchester City imekubali kichapo cha mabao 3 kwa 2 wakiwa ugenini wakicheza dhidi ya Norwich City, Mechi ya Chelsea imamemalizika kwa wageni Chelsea kushinda mabao 5 kwa 2 dhidi ya Wolverhampton Wanderers, Tottenham Hotspur wameitandika Crystal Palace mabao 4 kwa nunge.
Mabingwa wa Ulaya Liverpool wamecheza dhidi ya Newcastle na kushinda mabao 3 kwa 1, huku Mashetani wekundu Manchester United ikishinda bao moja kwa bila dhidi ya Leicester City kwa bao la mkwaju wa penati likifungwa na Marcus Rashford dakika ya 8.
Mechi mbili kupigwa Jumapili AFC Bournemouth wakiwakaribisha Everton saa 10 jioni huku Arsenal wakiwa wageni wa Watford mechi kupigwa saa 12 jioni.