Mashindano ya Kikapu kugombea Kombe la Taifa 2019 (Mtaka Basketball Taifa Cup) yamemalizika leo kwa mchezo wa fainali uliochezwa kati ya Arusha na Mwanza ambapo Arusha wameshinda 69 – 47.
Mchezo huo ilikuwa ufanyike jana 31 Dec 2019 lakini ulishindwa kuendelea kutokana na mvua kubwa iliyonyesha na ukaahirishwa na kufanyika leo mapema
Mchezaji nyota wa Mashindano hayo (MVP) ni Ally Mohamed kutoka Arusha ambaye pia amechukua tuzo ya mfungaji bora (Top Scorer) wa mashindano hayo, mlinzi bora (Best Defender) wa mashindano ni Abdul Kiango kutoka Arusha na timu yenye nidhamu ni Simiyu.
Pia kupitia mashindano hayo wachezaji nyota 12 (All Stars) walitangazwa ambao ni:
1)Ally Mohamed (AR)
2)Ally Buruba (MWZ)
3)Bahati Jacob (SHY)
4)Yohana Walwa(SHY)
5)John Samweli (SIM)
6)Francis Makuru (MARA)
7)Tyrone Martin (AR)
8)David Godfrey (AR)
9)Peter Jangu (MWZ)
10)Haji Mbegu (AR)
11)Ladislaus Lusajo (SIMY)
12)Amon Semberya (MWZ)