Mashabiki elfu 17 tu kushuhudia mpambano Lake Tanganyika

0
183

Mashabiki elfu 17 pekee ndio wataruhusiwa kuingia ndani ya uwanja wa Lake Tanganyika mkoani Kigoma, kushuhudia mpambano wa watani wa jadi Simba na Yanga siku ya Jumapili.

Mkuu wa mkoa wa Kigoma, Thobias Andengenye amesema wamepunguza idadi ya mashabiki kuingia ndani ya uwanja ili kuthibiti maambukizi ya ugonjwa wa corona.

Pia amesema kila atakayeingia uwanjani lazima awe amechukua tahadhari ikiwa ni pamoja na kuvaa barakoa na kunawa mikono.

Andengenye amesema wameandaa utaratibu mzuri wa kuweka mapipa ya maji nje ya uwanja huo wa Lake Tangnyika, ili kuwawezesha wanaoingia uwanjani kunawa mikono.