Manchester City watetea Ubingwa Ligi kuu England

0
277

Manchester City wametetea ubingwa wa ligi kuu England kwa kumaliza katika nafasi ya kwanza ya msimamo wa ligi hiyo wakimaliza na jumla ya alama 98 katika michezo 38 ya ligi.

Man City inachukua ubingwa huo huku Liverpool ikimaliza katika nafasi ya pili wakiwa na alama 97 na kushindwa tena kutimiza ndoto ya kutwaa taji hilo baada ya kulikosa kwa muda mrefu sasa.

Nafasi ya tatu imechukuliwa na Chelsea yenye alama 72 huku nafasi ya nne ikichukuliwa na Tottenham yenye alama 71, Arsenal wameshika nafasi ya 5 baada ya kupata alama 70 na Manchester United imeangukia nafasi ya 6 wakiwa na 66.