Manchester City mabingwa EPL

0
278

Klabu ya soka ya Manchester City imefanikiwa kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya England (EPL) kwa msimu wa mwaka 2020/21 baada ya mahasimu wao Manchester United kupigwa mabao 2-1 na Leicester City, hivyo kuwahisha sherehe za ubingwa.

Man City imetwaa kombe hilo mara tatu ndani ya misimu minne ikiwa na alama 80 ambazo haziwezi kufikiwa na timu nyingine yoyote, huku bado ikiwa na michezo mitatu mkononi.

Kombe hilo la 10 kwa Pep Guardiola tangu alipochukua usukani wa Manchester City limekuja wiki moja baada ya klabu hiyo kujihakikishia nafasi kwenye fainali ya Ligi ya Mabingwa Barani Ulaya (UCL), baada ya kuindoa Paris Saint-Germain ya Ufaransa kwa jumla ya magoli 4-1.