Man U yapata kibarua kizito kutoka kwa Rochdale

0
1232

Manchester United imelazimika kusubiri hadi kwenye mikwaju ya penati ili kusonga hatua inayofuata ya michuano ya kombe la Carabao, linalohusisha timu zinazoshiriki Ligi za England, baada ya kulazimishwa sare ya kufungana bao moja kwa moja kwenye muda kawaida na timu ya Rochdale.

Kinda Mason Greenwood wa Manchester United aliitanguliza timu yake kwa kufunga bao kwenye dakika ya 68 kabla ya kinda wa miaka 16, Luke Matheson hajaisawazishia timu yake ya Rochdale kwenye dakika ya 76.

Mchezo huo ukaenda kwenye changamoto ya mikwaju ya penati ambapo Manchester United ikapeta kwa kushinda mikwaju Mitano kwa Mitatu ya Rochdale.

Kwenye matokeo mengine, Chelsea imetinga kwa kishindo kwenye hatua ya Nne ya michuano hiyo kwa kuibugiza Grimsby Town mabao Saba kwa Moja.

Nao Liverpool wamesonga mbele kwa kuitungua Milton Keynes Dons mabao mawili kwa nunge.