Man U yaibamiza Liverpool Old Trafford

0
280

Wenyeji Manchester United wamepata ushindi wa kwanza katika Ligi Kuu ya England msimu huu baada ya kuichapa Liverpool mabao 2-1 Uwanja wa Old Trafford Jijini Manchester.

Mabao ya Manchester United yamefungwa na Jadon Sancho dakika ya 16 akimalizia pasi ya Malacia na Marcus Rashford dakika ya 53 akimalizia pasi nzuri ya Anthony Martial.

Nyota wa Misri, Mohamed Salah akaifungia bao la kufutia machozi dakika ya 82 akimalizia mpira uliookolewa na kipa David De Gea kufuatia pigo la Carvalho.

Mechi mbili za mwanzo za United chini ya kocha mpya, Eric ten Hag ilifungwa 2-1 na Brighton & Hove Albion hapo hapo Old Trafford Agosti 7 na 4-0 na Brentford ugenini Agosti 13, wakati Liverpool ilitoa sare zote, 2-2 na Fulham ugenini Agosti 6 na 1-1 na Crystal Palace nyumbani.