Mamia wamuaga Hans Poppe

0
2585

Mwili wa aliyekuwa mjumbe ya Bodi ya Wakurugenzi ya klabu ya Simba, na Mwenyekiti wa kamati ya usajili ya timu hiyo Zacharia Hans Poppe, umeagwa hii leo katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam.
 
Akiwasilisha salamu za Serikali wakati wa shughuli hiyo, mkuu wa wilaya ya Ilala,  Ng`wilabuzu  Ludigija ameitaka klabu ya Simba na Wanamichezo wote kumuenzi  marehemu Hans Poppe kwa kufanya yote aliyoyaanzisha kwa manufaa ya soka la Tanzania.
 
Zakaria Hans Poppe aliyekuwa kapteni mstaafu wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ)  alifariki dunia ijumaa ya tarehe 10 mwezi huu katika hospitali ya Aga Khan mkoani Dar es Salaam alikokuwa akipatiwa matibabu.