Majogoo ya Jiji waendelea kuwika England

0
858

Mabingwa wa Ulaya Liverpool wameendeleza ushindi katika michezo yao ya Ligi baada ya kutoka nyuma kwa bao moja bila dhidi ya Aston Villa kwa bao lililofungwa na Trezeguet mnamo dakika ya 21

Mchezo ulikuwa mgumu kwa Liverpool lakini kupitia kwa Robertson mnamo dakika ya 87 akarudisha matumaini kwa kupachika bao la kusawazisha,

Sadio Mane akapigilia msumari wa mwisho dakika ya tisini na kufanya mchezo huo kumalizika Liverpool ikipata ushindi wa Mabao mawili kwa moja dhidi ya Aston Villa na kufikisha alama 31 katika msimamo wa Ligi ikiendelea kuwa kinara.