Majeraha yasababisha Salah kukosa michezo miwili

0
1197

Nyota wa timu ya Taifa ya Misri na klabu ya Liverpool, – Mohamed Salah atakosa michezo miwili ya timu yake ya Taifa ya kufuzu kwa fainali za mataifa ya Afrika (AFCON) kutokana na kuuguza majeraha.

Idara ya Madaktari wa timu ya Taifa ya Misri imethibitisha kuwa nyota huyo wa Liverpool mwenye umri wa miaka 27 hali yake haijatengamaa, baada ya kupata majeraha madogo alipokuwa akiitumikia klabu yake wikiendi iliyopita.

Salah atakosa michezo ya kundi G ya kufuzu AFCON ambayo ni dhidi ya Kenya utakaochezwa kesho na mchezo dhidi ya Comoro utakaochezwa Novemba 18.

Kiongozi wa Madaktari hao wa timu ya Taifa ya Misri Dkt Mohamed Abul – Ela amesema kuwa, Mohamed Salah hajawa tayari kucheza mechi za ushindani kwa sasa huku akiwa anafanya mazoezi chini ya uangalizi maalumu wa matabibu hao.