Mahrez atimkia Saudi Arabia

0
207

Winga wa Algeria na Manchester City, Riyad Mahrez amejiunga Al-Ahli ya Saudi Arabia kwa uhamisho wa shilingi bilioni 94.5.

Nyota huyo ambaye bado alikuwa na mkataba wa miaka miwili ya City, anaongeza idadi ya majina makubwa ya wachezaji ambao wamejiunga Ligi Kuu ya Saudia.

Katika ujumbe wake wa kuaga mashabiki na timu hiyo amesema ilikuwa heshima kwake kuichezea Man City fursa iliyomwezesha kupata kumbukumbu zitakazodumu naye milele.

Kwa miaka mitano aliyoitumikia City ameiwezesha kushinda mataji 10, msimu wa mwisho ukiwa wa mafanikio zaidi ambapo walishinda makombe matatu, Ligi Kuu ya England, FA, Ligi ya Mabingwa.