Mabingwa CECAFA U23 kupokelewa kesho JNIA

CECAFA - U23

0
238

Mabingwa wa michuano ya Mataifa ya Afrika Mashariki na kati kwa vijana chini ya miaka 23 ( CECAFA CHALLENGE U-23 ) timu ya Taifa ya Tanzania na benchi zima la ufundi wanatarajia kurudi nchini siku ya Jumapili saa kumi na mbili na nusu asubuhi

Mabingwa hao wanatarajia kuwasili uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere JNIA kwa ndege ya Ethiopian Airlines

Tanzania imetwaa kombe hilo baada ya kuibamiza timu ya taifa ya Burundi kwa mikwaju ya penati 6 kwa 5 baada ya kutoka sare ya bila kufungana ndani ya dakika tisini