Kampuni ya Fenway Sports Group (FSG) ambayo ni wamiliki wa klabu ya Liverpool, wameiweka klabu hiyo ya Ligi Kuu England sokoni na wanakaribisha ofa kwa wanaohitaji kuinunua.
FSG inaipiga mnada klabu hiyo baada ya kudumu nayo kwa takribani miaka 12 tangu ilipoinunua kutoka kwa George Gillette na Tom Hicks mwaka 2010.
Mabingwa hao mara 6 wa Ligi ya Mabingwa Barani Ulaya, wameanza msimu huu kwa kusuasua kwenye Ligi ya EPL licha ya kutinga hatua ya 16 ya UCL.