Vijana hao wa The Gunners wametwaa mara 13 ubingwa wa kombe la FA, huku Manchester United wakitwaa taji hilo mara 12.
Michezo mingine ambayo inatolewa macho na wapenzi wa soka ni Tottenham hotspur, watakaokuwa ugenini kuikabili Crystal Palace, Manchester City wao watakuwa nyumbani dhidi ya Burnley wakati Chelsea watakuwa katika dimba lao la Stamford Bridge jijini London, kuwakabili Sheffield Wednesday baada ya timu hizo kupambana na kupatika mshindi siku ya jumatano.