Timu ya Liverpool imeibamiza AFC Bournemouth mabao 9 kwa bila katika mchezo wa ligi kuu England uliopigwa katika dimba la Anfield
Katika mchezo mwengine Manchester united imechomoza na ushindi wa bao moja kwa bila ugenini wakicheza dhidi ya Southampton
Chelsea wakiibamiza Leicester city mabao 2 kwa 1, Arsenal wakiendelea kutakata kileleni baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 2 kwa 1 dhidi ya Fulham na kuendelea kushika usukani wa ligi hiyo wakiwa na alama 12 baada ya kucheza michezo 4 na kushinda mechi zote
Manchester city wapo nafasi ya pili kwa alama 10 baada ya kuitandika Crystal Palace mabao 4 kwa 2 wakiwa nyumbani Etihad, Leeds wameambulia kichapo cha bao moja kwa bila dhidi ya Brighton huku Everton wakilazimisha sare ya bao 1 kwa 1 dhidi ya Brentford
Leo timu ya Aston Villa itakipiga dhidi ya West Ham United, Wolves wakicheza dhidi ya Newscastle na Nottingham Forest watacheza dhidi ya Tottenham Hotspur