Majogoo wa jiji Liverpool wamekiona cha moto usiku wa jana, kwa kutandikwa bao moja kwa bila na Southhampton katika mchezo wa Ligi Kuu ya England uliochezwa kwenye dimba la St. Marry’s.
Bao la mapema dakika ya pili lililofungwa na Danny Ings limetosha kuwapa wateule hao alama tatu muhimu, na kupanda hadi nafasi ya sita kwenye msimamo wa Ligi ya England wakifikisha alama 29.
Licha kipigo hicho, Liverpool bado wanaendela kusalia kileleni wakiwa na alama 33 baada ya kucheza michezo 17, alama sawa na Manchester United waliopo katika nafasi ya pili lakini United wakiwa wamecheza michezo 16.