Vinara wa ligi kuu soka England Liverpool imeendelea kujikita kileleni mwa ligi hiyo baada ya kuibuka na ushindi ugenini wa mabao 2 kwa 1 dhidi ya Wolverhampton wanderers katika uwanja wa Molineux
Liverpool walianza kufunga kupitia kwa Jordan Henderson dakika ya 8 kisha Wolves kusawazisha dakika ya 51, lakini kabla ya kipenga cha mwisho Roberto Firmino anaiandikia bao la ushindi Liverpool dakika ya 84 na kuifanya Liverpool kuongeza alama 3 muhimu hivyo kufikisha alama 67 katika msimamo wa ligi huku wakiwa wamekwisha cheza michezo 23
Wolves yenyewe inabaki nafasi ya 7 ikiwa na alama 34 baada ya kucheza michezo 24 wakiwa alama sawa na Tottenham pamoja na Manchester United