Katika Michezo ya Ligi kuu England iliyopigwa weekend hii Chelsea imeonesha ubabe wake mbele ya Arsenal baada ya kutoka nyuma kwa bao moja bila na kushinda 2 kwa 1
Mchezo wa Pili Liverpool imetumia vyema uwanja wa nyumbani baada ya kushinda bao 1 kwa nunge dhidi ya Wolverhampton wakiwa katika Dimba la Anfield
Bao la Liverpool limefungwa na Sadio Mane dakika ya 42 bao lililoamuliwa kwa usaidizi wa mfumo wa VAR huku Wolves nao wakikataliwa goli lao kupitia mfumo wa VAR baada ya mchezaji wao kuonekana ameotea
Kwa matokeo hayo Liverpool inazidi kujikita kileleni mwa ligi kuu baada ya kufikisha alama 55 baada ya kucheza michezo 19 ikiwa na mchezo mmoja kibindoni