Mabingwa wa Ulaya Liverpool imetoka nyuma kwa bao moja bila dhidi ya Tottenham Hotspur katika dimba la Anfield na kushinda jumla ya mabao mawili kwa moja katika mchezo wa Ligi Kuu England
Bao la kwanza kwa Tottenham likifungwa mapema dakika ya kwanza na mshambuliaji mahiri Harry kane, huku bao lakusawazisha la Liverpool likifungwa na Henderson na bao la pili likifungwa na Mohamed Salah kwa mkwaju wa Penalt
Liverpool inaendelea kuongoza Ligi hiyo ikiwa na alama 28 huku ikiwa haijapoteza mchezo hata mmoja katika michezo 10 iliyokwishacheza, ikishinda 9 na kutoka sare mchezo mmoja dhidi Manchester United.