Liverpool Mabingwa Ulaya

0
585

Majogoo ya Jiji Liverpool wanamaliza ukame wa mataji na kuwa mabingwa mara sita barani Ulaya baada ya kuitandika Tottenham mabao mawili kwa bila katika mchezo wa fainali wa ligi ya mabingwa Ulaya uliopigwa katika dimba la Wanda Metropolitano mjini Madrid

Bao la kwanza katika mchezo huo wa fainali limefungwa kwa mkwaju wa penalty na mchezaji Mohamed Salah dakika ya 2 huku Origi akiimaliza Tottenham kwa kupachika bao la pili dakika ya 87 na kufanya matokeo kuwa 2 bila hadi dakika 90 za mchezo huo.