Liverpool kutoana jasho na Flamengo

0
467

Majogoo wa Jiji Liverpool watamenyana na Flamengo ya Brazil katika mchezo wa fainali wa klabu bingwa ya Dunia utakaochezwa Jumamosi hii huko Qatar.

Liverpool ambao ni mabingwa wa Ulaya, wametinga hatua ya fainali baada ya kuinyuka Monterrey ya Mexico kwa mabao mawili kwa moja katika mchezo wa Nusu fainali.

Bao la dakika za mwisho la Roberto Firmino limeipeleka Liverpool fainali baada ya Funes Mori kuisawazishia Flamengo katika dakika ya 14 ambapo liverpool walitangulia kupata bao la kuongoza kupitia kwa Nabil Keita katika dakika ya 11.

Hii ni mara ya pili kwa Liverpool kutinga hatua ya fainali ya kuwania taji la klabu bingwa ya Dunia, ikiwa ni timu ya kwanza kutoka England kuingia katika fainali ya kuwania ubingwa huo mara mbili.